Wajawazito wabebwa kwa Mkokoteni Km 12, kufuata huduma ya Afya Songwe

WANANCHI wa kijiji cha Chole kata ya Mkomba wilaya ya Momba mkoani Songwe wakiwemo wazee na wajawazito wanatumia usafiri wa mkokoteni wa kukokotwa na Ng’ombe umbali wa kilimeta 12 kufuata huduma za matibabu kutokana na kutokuwa na zahanati ambapo kata nzima ina Zahanati mbili zikiwa na wahudumu watatu wa afya hali inayowapa wakati mgumu akina mama wengi hususani wajawazito, wazee na watot
Wakizungumza kijijini hapo,wakazi wa kijiji hicho,wamesema ukosefu wa barabara na zahanati katika kijiji chao,ni moja ya sababu ya kukumbwa na kadhia hiyo,ikiwemo kupoteza maisha ya watoto wao pindi wanapo safiri kwa kutumia mkokoteni unao kukokotwa na Ng’ombe umbali wa kilometa 12 kufuata huduma za matibabu, wakati wakijifungua kwa shida wakiwa njiani,huku wakiiomba serikali kuwaondolea tatizo hilo.

Mwenyekiti wa kijiji cha chole Dmian Sichila anakiri kupokea taarifa za vifo vya akina mama na watoto kutokana na kukosa huduma za matibabu zinazofuatwa umbali mrefu, huku diwani wa kata ya Mkomba Colletha Mwanselela akisema kata nzima ina zahanati mbili na wauguzi watatu hivyo kiwango cha utoaji huduma kuwa duni,hivyo wameamua kujenga zahanati ya kijiji na kuiomba serikali kuunga mkono jitihada zao ikiwemo kuwapatia wauguzi.

Mathew Chikoti ni wenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Momba licha ya kupongeza jitihada za wananchi hao ameeleza mpango wa halmashauri kuunga mkono jitihada hizo ikiwemo kupeleka watumishi huku Juma Irando,mmkuu wa wilaya ya Momb,amesema amekuwa akikumbushia kila mara idara ya utumishi kupeleka watumishi wa kutosha vijijini kisha akaeleza mpango wa serikali kukabiriana na hali hiyo.

No comments: