Mtatiro afunguka kukamatwa kwa Peter Msigwa

Saa chache baada ya Mbunge Iringa mjni Peter Msigwa, Julius Mtatiro ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Facebook

"Kukamatwa kwa Mhe. Peter Msigwa, mbunge wa Iringa Mjini ni mwendelezo wa Uimla na Ukandamizaji unaofanywa na Serikali ya sasa dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani. Na ni njia ile ile ya sasa ya kukandamiza demokrasia nchini."


Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Kamishna wa polisi Julius Mjengi ameueleza mtandao huu kuwa Msigwa alikuwa na mkutano wa hadhara leo Septemba 24, katika eneo la Mlandege mkoani humo ambapo anadaiwa kutumia lugha na matamshi ya uchochezi katika hotuba yake.

No comments: