Kinachosababisha Mahusiano Mengi ya Kimapenzi kufa Ni Hiki

Tumekuwa ni mashuhuda wazuri tukishuhudia mahusiano ya kimapenzi yanapoanza, huwa yaanaanza kwa mbwembwe nyingi sana, lakini yanapokuja kufa huwa ni kimya kimya, wale wale ambao tuliwashuhudia wakitembea kwa pamoja mara baada ya mahusiano hayo kufa, tumekuwa tukiona kila mtu yupo kivyake.


Licha ya kuendelea kushuhudia hivyo, ukichukunguza kwa umakini sababu ya kufa kwa mahusiano hayo utakuja kugundua kitu kimoja kikubwa ambacho kimesababisha kufa kwa mahusiano hayo ni; uwongo unapobadilika kuwa ukweli.
Hii ni sababu kubwa sana ambayo husababisha mahusiano mengi kufa, na sababu hii ndiyo husababisha mtafaruko mkubwa katika mahusiano yaliyo mengi. Hii ni kwa sababu watu wengi ambao wanaingia katika mahusiano hutumia njia ya kudanganya ili aweze kumpata fulani, kwa sababu katika sayari ya leo bila uongo mapenzi hayaendi.
Hii ipo wazi, ya kwamba mapenzi ni uongo ambao hufanana na ukweli. Wakati mwingine kabla hujaanza mahusiano na mpezi wako, huwa kunakuwapo na ahadi nyingi sana ambazo zipo baadhi huwa ni za ukweli na zipo nyinginezo ambazo huwa ni za uongo.
Na hizo nyinginezo za uongo pale ambapo inakuja kugundulika ya kwamba zilikuwa za uongo ndipo unakuwa mwanzo wa mahusiano hayo kufa, unakuta mtu wakati wa kumtongoza msichana fulani anamuahidi vitu vingi vya uongo msichana huyo, na msichana huyo pasipo kujua anajikuta anakubali huku akitegemea kwamba ahadi zote alizoahidiwa na mpenzi wake zitakuja kuwa ukweli, mwisho wa siku ahadi hizo zinabaki kuwa stori mwisho wa siku msichana huyo anaamua kuachana na mwanaume huyo.
Kwa mfano unakuta mtu anamwambia mtu ukiwa na mimi nitakupa nyumba, gari, fedha lakini baada ya muda kadhaa kupita vitu hivyo vinaishia kwenye maneno tu.
Na sababu nyingine ambayo husababibisha mahusiono mengi kufa ni kitu ambacho kinaitwa matarajio. Na matarajio hayo huwa katika ahadi ambazo zilikuwepo wakati awali. Unakuta mtu kabla hajaingia katika mahusiano na mtu fulani anakuwa anatarajia kupata kitu fulani kutoka kwa mtu huyo, mwisho wa siku kitu hicho ambacho alikuwa anatarajia anakuta hakipo.
Hivyo akikuta hakipo mwisho wa siku anaamua kuachana na mtu huyo na kwenda kwa mtu mwingine. Hivyo mambo makubwa ambayo hubomoa mahusaiano ya kimapenzi ni hayo ambayo nimeyaeleza.

No comments: