RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Magufuli ametangaza kutoa nafasi 3,000 kwa vijana waliopitia mafunzo ya ukakamavu kujiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza baada ya kuwatunuku nishani ya Luteni Usu maofisa 422 wa jeshi, Magufuli amesema lengo la kutoa nafasi hizo ni kuhakikisha jeshi linakuwa na askari wa kutosha.
“Jeshi haliwezi kuwa na maofisa tu, tutaongeza na askari wa kawaida, natangaza rasmi kuwa, nitaajiri wanajeshi 3,000, nitazingatia waliohitimu vyema mafunzo ya JKT, tunataka tujenge jeshi la kisasa.” alisema Magufuli na kuongeza.
“Kuna mmoja alikuwa anasema habari za Jeshi tukamkamatia Mbeya tukampeleka jeshini akajifunze kuwa msemaji wa jeshi. Wakati nateua Wakuu wa Mikoa Wanajeshi watu waliongea, lakini mimi napenda wanajeshi sababu mambo yao yanakwenda haraka.”
Rais Magufuli amewataka Watanzania kutoa ushirikiano kwa jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili viendelee kufanya kazi yao kwa ufanisi, amani na utulivu viendelee kutawala nchini.
No comments: