RATIBA YA MSIMU WA LIGI KUU TANZANIA BARA

vpla-426x360-696x588
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 23, mwaka huu kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja tofauti hapa nchini.



Kesho Jumamosi Young Africans itacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Mwadui ya Shinyanga katika mchezo utaofanyika Uwanja wa Mwadui.



Mchezo mwingine, utakutanisha timu za Majimaji itakayokuwa mwenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Mechi zote hizo zitaanza saa 10.00 jioni.



Jumapili Septemba 24, mwaka huu kutakuwa na michezo minne ambako Ruvu Shooting itaialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikicheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. Mechi hizo pia zitaanza saa 10.00 jioni.

Michezo mingine itakuwa ni Singida United itakayoialika Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma saa 10.00 jioni kabla ya Azam kuialika Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi katika mchezo utakaoanza saa 1.00 jioni

Na ufuatao ni msimamo wa Ligi hiyo baada ya mchezo kati ya Mbao FC dhidi Ya Simba Sc.

IMG-20170922-WA0013

No comments: