SIKU chache baada ya baba mzazi wa mtoto wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto, kujitokeza hadharani na kukiri mtoto ni wake, ghafla, katika hali ya kushangaza zikasambaa picha mitandaoni zikimuonyesha mwanamitindo huyo akiwa katika pozi za mahaba na mdau wa muziki, Petitman Wakuache. Baada ya kuziona picha hizo Petit ameibuka na kutoa kauli nzito.
Kila binadamu ana jana yake, leo na kesho ambayo ni fumbo, kwa sababu ameshasema kwamba picha hizo ni jana yake, ambayo haiuhusiani kabisa na leo yake. Basi ni vyema hao wanaohusika na usambazaji wa picha hizo, mkasitisha zoezi hilo, kwani Petit ni mume na baba wa familia kwa sasa.
Mobeto naye ana maisha yake mengine kabisa, kwa hiyo kuvujisha picha hizo kunaweza kusababisha migogoro katika familia hizi mbili ambazo zina uhusiano wa karibu.
No comments: