Beki wa kushoto wa Manchester City Benjamin Mendy hatoshiriki katika mechi ya vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Shaktar Donetsk katika uwanja wa Etihad kutokana na jeraha la goti.
Mendy alitolewa nje wakati wa ushindi wa City wa 5-0 dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumamosi na anatarajiwa kutibiwa mjini Barcelona na mtaalam.
Kiungo wa kati IIkay Gundogan ana jeraha la goti naye beki Vincent Kompany akiugua jereha la nyonga na wote hawatashiriki.
City iliwafunga Feyenoord 4-0 katika mechi ya ufunguzi na klabu hiyo inaongoza jedwali la ligi ya Uingereza wakiwa wamefunga mabao 27 katika mechi nane kufikia sasa msimu huu.
''Tunapocheza nyumbani tunahisi tutafunga mabao mengi'', alisema mkufunzi wa City Pep Guardiola.
''Ni nafasi ngapi tutatengeza na kufungwa ni sawa na msimu ulioipita.Uthabiti unaweza kushuka''kwa hivyo lazima tutahadhari''.
No comments: