
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandima raia wa Zambia, amesema kuwa beki wake Kelvin Yondani ndiye aliyewabeba mpaka wakaibuka na ushindi dhidi ya Ndanda, jana Jumamosi.

Katika mchezo huo, Yanga ilijipatia bao lake hilo pekee kupitia kwa Ibrahim Ajibu dakika ya 34.
Lwandamina amesema: “Kwangu Yondani ndiye ‘man of the match’ dhidi ya Ndanda kwani alicheza vizuri sana kwenye nafasi yake kwa kulinda na kupandisha mashambulizi.
“Hata bao alilofunga Ajibu ametoa pasi yeye, hivyo binafsi nampongeza kwa kucheza vizuri.”
No comments: