Hakuna ndoa kati ya Kylie Jenner na Travis Scott ni mtoto tu

Huwenda watu walitegemea kuona ndoa kati ya Kylie Jenner na Travis Scott, ila kwa hali ilivyo wawili hao hawatarajii kufunga ndoa japo kuwa wanatarajia kupata mtoto.

Image result for Kylie Jenner na Travis Scott picha

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kimeeleza kuwa Kylie Jenner na Travis Scott, hawajaongea jambo lolote kuhusiana na kufunga ndoa ila wanajua kuhusu umuhimu wa malezi kwa watoto wake.
“They’re still trying to figure out their relationship,” kimeongea chanzo hicho kupitia mtandao wa TMZ.
Pia chanzo hicho kimeongeza kuwa licha ya kuwa mrembo huyo ana ujauzito wa miezi mitano ila ana hofu ya kuingia katika ndoa haraka kutokana na yaliyowakuta ndugu zake  Kim na Kourtney.
Kylie anaingia katika orodha ya Kardashian wataoongeza familia ifikapo mwakani kwani tayari Kim ana tarajia mtoto wa tatu huku naye Khloé akitarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mcheza kikapu wa NBA, Tristan Thompson

No comments: