Diego Costa aishukuru Chelsea

Image result for diego costa
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea aliyerejea nyumbani Atletico Madrid, Diego Costa amesema hawezi kuisahau Chelsea kwa muda ambao amekuwa kwenye timu hiyo.

Diego ameishukuru Chelsea na kueleza hisia zake juu ya mafanikio aliyopata akiwa na klabu hiyo katika miaka yake mitatu ya kuwa darajani.

“Siwezi kusahau miaka yangu mitatu ndani ya Chelsea, nimecheza mechi 120 nimefunga mabao 59 na kusaidia mengine 24 hakika naishukuru klabu na watu wote tulioshirikiana kufanikisha hayo”, amesema Diego Costa.

Costa alifunga mabao 20 kwenye misimu ya 2014-15 na 2016-17 pamoja na kuisaidia timu yake kushinda ubingwa wa EPL mara 2 chini ya makocha wawili ambao ni Mourinho aliyemsajili kutokea Atletico Madrid pamoja na Antonio Conte.

No comments: