Beki wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Manchester City, Benjamin Mendy anatarajiwa kuwasili Barcelona kwaajili ya matibabu ya goti.
Akizungumza kabla ya mchezo wa Klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya timu ya Shakhtar Donetsk, Pep Guardiola amependekeza, Mendy mwenye umri wa miaka 23, kuanza mazoezi Jumatatu ya wiki ijayo.
Full-back huyo wakimataifa wa Ufaransa amecheza katika ushindi wa mabao 5-0 wakati timu yake Manchester City ilipocheza dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumamosi.
Mendy ambaye amesajiliwa na City kwa dau la paundi milioni 52 akitokea Monaco atasafiri kuelekea Barcelona kukutana na Ramon Cugat, rafiki wa karibu na Guardiola ambaye ndiye aliyewatibu wachezaji wa klabu hiyo, Vincent Kompany na Kevin de Bruyne msimu uliyopita.
No comments: