Botswana: Almasi iliyopatikana yauzwa kwa dola milioni 53


Almasi yenye haijakatwa ya ukubwa wa mpira wa tenisi, iliyopatikana kwenye mgodi wa Korowe nchini Botswana mwezi Novemba mwaka 2015, imeuzwa na kampuni yenye makao yake nchini Canada ya Lucara Diamond kwa kima cha dola milioni 53.

Almasi hiyo yenye karati 1,109 ambayo kwa sasa ndiyo kubwa zaidi ambayo bado haijakatwa duniani, ilinunuliwa na kampuni ya Uingereza ya Graff Diamonds kwa dola 47,777 kwa kila karati na sasa itakatwa.

Kampuni ya Canada awali ilijaribu kuiuza almasi hiyo kwenye mnada mwezi Juni mwaka 2016, lakini haikupata bei ilikuwa inahitajika.

Almasi hiyo kwa jina Lesedi La Rona au mwangaza wetu kwa lugha ya taifa nchini Botswana inatajwa kuwa ya miaka bilioni 2.5 hadi bilioni 3.

Kampuni ya Laurence Graff, ilisema kuwa ni hashima kubwa kuwa sasa inamiliki almasi hiyo

No comments: