Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten imesema kuwa klabu ya Yanga ilipaswa kusafiri leo lakini imeshindikana kutokana na mabadiliko ya ratiba ya ndege hivyo timu yao itaondoka kesho asubuhi kuelekea Bukoba.
"Mabadiliko ya ratiba ya ndege si jambo geni sisi tulijiandaa kwenda leo lakini tumepewa taarifa kuwa ratiba yetu imebadilika mpaka siku ya kesho asubuhui ndiyo tutasafiri, mwalimu anaelewa utaratibu ambao upo maana si mara moja safari za ndege kuhairishwa jambo jema kwamba yeye mwenyewe kapata taarifa na ameridhia na yeye amejindaa na kuwaanda wachezaji wake kwa ajili ya safari kesho asubuhi" alisema Dismas .
Aidha Dismas amedai kuwa wao kama klabu jukumu lao ni kuweka mazingira mazuri kwa timu na wachezaji ili waweze kupata pointi tatu muhimu Kagera dhidi ya Kagera Sugar .
"Mchezo wa Bukoba tunacheza ugenini kwa hiyo watu wanahitaji kuwa sawa ili kimwili na kiakili kupambana kuweza kupata matokeo mazuri, siku zote mpira wa miguu haijalishi unacheza nyumbani au ugenini maandalizi unayokuwa umeyafanya ndiyo yanaleta matokeo, kwa kuwa mpira wa miguu unachezwa uwanjani" alisema Dismas Ten
No comments: