Wachina waliofanyiwa ‘surgery’ kubadilisha sura, wazuiliwa kuondoka Airport

Wachina watatu wamezuiliwa nchini Korea Kusini baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo kwenye sura zao.

Wachina hao ambao walisafiri kutoka China kwenda Korea Kusini kwa lengo la kubadilisha sura zao, wamekataliwa kuondoka nchini humo kurudi kwao baada ya maafisa usalama kushindwa kuwatambua kwa kuwafananisha sura zao za kwenye passport za kusafiria siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita.
Taarifa za wachina hao kuzuiliwa nchini Korea Kusini zilianza kusambaa mtandaoni Jumapili iliyopita baada ya mtangazaji maarufu nchini humo, Jian Huahua kuvujisha picha za wachina hao kwenye mtandao wa Twitter na kuandika “ Baada ya kusafiri kwa ajili ya matibabu ya upasuaji, Wachina hawa wamezuiliwa uwanja wa ndege“.
Baada ya posti hiyo kwenye mtandao wa Twitter taarifa zikaanza kusambaa kwenye vyombo vya habari na tayari serikali nchini China imethibitisha taarifa hizo za kuzuiliwa kwa wachina hao.


Mpaka sasa bado wamezuiliwa kuondoka nchini Korea Kusini na jitihada za kidiplomasia za kuwarejesha zinaendelea.

No comments: