Msanii wa muziki wa kizai kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, ameweka wazi sababu ya kuuza magari yake na kuonekana akipanda daladala, na kukiri kweli ameuza magari.
Akiongea na mwandishi wa East Africa Television, Nay amesema ameuza magari hayo kwa sababu mbalimbali ambazo anazijua yeye, hivyo watu wasishangae wakimuona akikatisha mtaani kwa mguu na wasisite kumpa lifti kwenye magari yao.
"Kila mtu anazungumza lake ujue, lakini kama kuuza nimeuza kwa sababu zangu za msingi, nimemua kuachana na magari nipande daladala na bajaji, na hayo ndio maisha ambayo nimekulia, unajua mimi nimezaliwa kwenye maisha ya kawaida na mtaa ndio umenilea, kwa hiyo watu wasichoke kunipa lifti wakiniona, au wasishangae siku wakiniona natembea kwa mguu", amesema Nay wa Mitego.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kuwa msanii huyo amefulia kiasi cha kufikia uamuzi wa kuuza magari yake, na baadhi ya nyumba ambazo alikuwa akimiliki, na kuonekana akitembea kwa bajaji kitu ambacho sio cha kawaida kwake.
No comments: