Yanga Wamtaja Mrithi Wa Tshishimbi Mechi Dhidi Ya Mtibwa Sugar.

Kabamba%2BTshishimbi

Baada ya kiungo mkabaji wa klabu ya Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi kuonyeshwa kadi tatu za manjano na kulingana na sheria na kanuni za soka kiungo huyo hataruhusiwa kucheza mchezo mmoja.

Tshishimbi ataukosa mchezo kati ya Yanga  dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo utakaochezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Hata hivyo kocha mkuu wa klabu hiyo amepanga kumtumia kwa mara ya kwanza kiungo Pius Buswita kuziba pengo la Tshishimbi katika mchezo huo.

No comments: