Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba SC, Shiza Kichuya anatarajiwa kurejea dimbani Jumapili hii kuwavaa Stand United katika mchezo wa mzunguko wa tano baada ya kupona majeraha aliyoyapata katika mechi iliyopita dhidi ya Mbao FC.
Hayo yamewekwa wazi na Afisa wa Habari wa wekundu wa Msimbazi, Haji Manara ambaye amesema winga huyo mwenye msaada mkubwa katika kikosi hicho ameanza mazoezi mepesi tokea jana na wenzake.
"Hali ya kikosi cha Simba hadi sasa ni nzuri, tulikuwa na majeruhi mmoja Shiza Kichuya ambaye tayari ameshaanza mazoezi, kwa hiyo kama kocha ataamua kumtumia siku ya Jumapili atatumika, tunawaomba watu wa Kanda ya ziwa waje kuipa ushirikiano timu yao kama walivyo walivyofanya katika mechi dhidi ya Mbao FC", amesema Manara.
Simba SC inatarajiwa kushuka katika dimba la Kambarage Mkoani Shinyanga Oktoba mosi mwaka huu kuwavaa Stand United FC huku ikiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi nane, wakati Stand United FC ipo nafasi ya 12 ikiwa na alama tatu.

Related posts
Kichuya kurejea dimbani Jumapili
Reviewed by Informalblogsport
on
15:48
Rating: 5
No comments: