UWANJA WA SIMBA BUNJU UTABAKI KUMBUKUMBU


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amefichua kuwa ujenzi wa uwanja wao wa Bunju hautaendelezwa tena na umesimama kupisha kesi iliyopo mahakamani ambayo inawakabili viongozi wake wa juu, Evans Aveva na Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
Manara Alisema, “Kuhusiana na ukarabati wa uwanja wetu wa Bunju niweke wazi kwamba hauendelezwi kwa sasa ni kimya umesimama kupisha kesi iliyopo mahakamani hadi pale viongozi wetu wa juu Aveva na Kaburu watakapojuwa hatima ya kesi inayowakabili,”alisema Manara.
Simba ni miongoni mwa klabu vigogo nchini ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele kutokana na kutokuwa na uwanja wake. Tatizo kama hilo linawakabili pia watani zao Yanga.

No comments: