Ujerumani yapaa mpaka kombe la Dunia 2018


Germany walihitaji kutoka sare au kushinda kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018
Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Ujerumani wamefuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Urusi baada ya kulaza Ireland Kaskazini 3-1 mjini Belfast.
Sebastian Rudy alifunga bao dakika ya pili, Sandro Wagner akaongeza la pili baadaye, naye Joshua Kimmich akafunga la tatu mechi ikikaribia kumalizika.
Josh Magennis alifungia Ireland Kaskazini bao la kufutia machozi kwa kutumia kichwa dakika za lala salama.
Ujerumani wamefuzu wakiwa viongozi wa kundi lakini Ireland Kaskazini wanasalia bado na matumaini ya kufuzu kupitia mechi za muondoano za kufuzu Novemba.
Vijana hao wa Michael O'Neill watamaliza mechi zao Kundi C nchini Norway Jumapili, wakilenga kumaliza wakiwa miongoni mwa timu nane bora zitakazomaliza nafasi ya pili kati ya makundi tisa ya kufuzu.
Ireland Kaskazini wameshindwa mechi zao mbili kundini mikononi mwa Ujerumani

No comments: