Mtalii mmoja kutoka nchini Ufaransa aliyechukua hatua za haraka amesifiwa baada ya kulizui basi kupingirika chini ya mteremko katika milima ya Alps nchini Austria baada dereva wa abasi hilo kuzimia.
Gari hilo lilikuwa likipitia eneo la milima likiwa na abiria 21 wakati dereva mwenye umri wa miaka 76 alizimia.
Wakati basi lilikuwa likielekea chini ya mlima raia huyo wa Ufaransa alifaninikiwa kupiga breki.
Basi hilo liligonga kizuuzi kando ya barabara kisha likasimama. Watu wanne walipelekwa hosptalini.
Abiria raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 65 aliyekwa ameketi kando mwa dereva wakati aligonjeka karibu na mji wa Schwaz magharibi mwa Austria siku ya Jumamosi.
Alitoka kwa kiti chake wakati gari hilo lilikuwa linagonga kuzuizi cha mti kilicho kando ya barabara na kukanyaga breki.
Mwaka 2004 watalii watano waliuawa wakati basi liliacha barabara na kupingira chini ya mlima karibu ni kijiji cha Bad Dürrnberg nchini Austria.
No comments: