Michuano ya kuwania kufuzu kombe la dunia hapo mwakani nchini Urusi imeendelea tena usiku wa kumkia leo baada ya timu kadhaa za taifa kuingia uwanjani kutafuta tiketi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa na ya kwanza katika mchezo wa soka ikifuatiwa na klabu bingwa barani Ulaya.
Mchezaji wa taifa ya Uingereza, Harry Kane
Timu ya taifa ya Uingereza imechomoza na ushindi wa 1-0 mbele ya Slovenia kwa bao lililofungwa na nahodha wao, Harry Kane dakika za majeruhi na kuifanya kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urisi.
Uingereza ambayo ilishuka katika dimba la Wembley ilihitaji pointi mbili pekee ili kupata nafasi ya kushiriki katika michuano hiyo inayojumuisha mataifa mbali mbali duniani na hatimae Kane kufunga bao hilo katika dakika ya 94 ya mchezo wa kundi F.
Na timu ya Scotland imechomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Slovakia bao la dakika za mwisho la Martin Skrtel limefufua matumaini ya timu hiyo kwenda kombe la dunia baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi lao.
Wakati timu ya taifa ya Ujerumani ikiwa ugenini imechomoza na ushindi wa mabaoa 3-1 mbele ya Northern Ireland.
Matokeo ya michezo mingine ni kama ifuatavyo.
No comments: