Tuzo za Dunia:wakenya walibeba Afrika Mashariki kwa riadha

Wanariadha wawili raia wa Kenya wametajwa kuwania tuzo za dunia kwa mwaka 2017 hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa taifa pekee kutoka Afrika Mashariki kuingiza wanariadha katika tuzo hizo.


Elijah Manangoi ni mwanariadha pekee kutoka Kenya ambaye ametajwa kwenye orodha ya wanariadha 10 wa kiume na Hellen Obiri ambaye yumo katika orodha ya wanariadha kumi wa kike wanaowania tuzo hiyo.
Mbali na wakenya hao, pia yumo Muethiopia mmoja ambaye ni Almaz Ayana pamoja na wanariadha watatu kutoka Afrika Kusini akiwemo Caster Semenya.
Orodha kamili ya wanariadha hao wanaowania tuzo za dunia ni:-
Kwa upande wa Wanaume:
Mutaz Essa Barshim (Qatar); Pawel Fajdek (Poland); Mo Farah (Uingereza); Sam Kendricks (Marekani); Elijah Manangoi (Kenya); Luvo Manyonga (Afrika Kusini); Omar McLeod (Jamaica); Christian Taylor (Marekani); Wayde van Niekerk (Afrika Kusini); Johannes Vetter (Ugiriki).
Na kwaupande wa Wanawake:
Almaz Ayana (Ethiopia); Maria Lasitskene (Urusi); Hellen Obiri (Kenya); Sally Pearson (Australia); Sandra Perkovic (Croatia); Brittney Reese (Marekani); Caster Semenya (Afrika Kusini); Ekaterini Stefanidi (Ugiriki); Nafissatou Thiam (Ubelgiji); Anita Wlodarczyk (Poland).

No comments: