KWA TAKWIMU HIZI INASADIKIKA KUWA NDIO MCHEZAJI BORA KUWAHI KUTOKEA ULIMWENGUNI


Ni uzao wa mshambuliaji wa kikosi cha Brazil cha miaka ya 1930’s – João Ramos do Nascimento na mwanamama Celeste Arantes.
Ni baba wa watoto sita, Sandra Machado, Kelly Cristina, Flávia Kurtz, Edinho, Joshua na Celeste.
Inasadikika ndio mchezaji bora wa wakati wote wa soka, akiwa na rekodi ya kucheza jumla ya mechi 1363 na kufunga magoli 1281.
Ameshinda ubingwa wa dunia na Brazil mara 3 na Copa America mara 1. •Mfungaji bora wa muda wote wa Brazil (Magoli 95)
•Ana rekodi ya dunia ya kufunga hat tricks 92
•Mfungaji mdogo zaidi katika michuano ya kombe la dunia, mfungaji – miaka 17 na siku 239 (Brazil v Wales 1958)
•Mfungaji wa hat trick mdogo zaidi katika World Cup – miaka 17 na siku 244 (Brazil v France 1958)
•Mfungaji mdogo zaidi katika mchezo wa fainali ya Kombe la dunia na mshindi wa taji hilo – miaka 17 na siku 249.
Wazazi wake Dondinho na Celeste walimpa jina la Edson Arantes do Nascimento – ulimwengu wa soka unamtumbua kama #PELE – siku kama ya jana, Oktoba mwaka 1977 Pele alistaafu kucheza soka akiwa na klabu ya Cosmos ya Marekani.

No comments: