Mkuu na mwanzilishi wa mtandao wa Facebook ,Mark Zuckerberg, amebeza maoni ya rais Donald Trump dhidi ya mtandao huo kwamba umekuwa ukimpinga.
Zuckerberg amesema pande zote mbili za kisiasa nchini Marekani zilikuwa zikiutazama mtandao wa Facebook tofauti kutokana na kutofurahishwa na maoni yanayotolewa na watumiaji.
Ameongeza wakati wa uchaguzi Democrats wamewahi tuhumu mtandao huo kwamba unamsaidia Trump.
Mwanzilishi huyo wa Facebook amebainisha kuwa wakati wote wa uchaguzi mtandao wake ulifanya unachoweza kwa manufaa ya wapiga kura.
No comments: