Trump: Muuaji wa Las Vegas ana matatizo ya kiakili


Baadhi ya waliohudhuria tamasha hilo wakitoroka kufuatia shambulio la bwana PaddockHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBaadhi ya waliohudhuria tamasha hilo wakitoroka kufuatia shambulio la bwana Paddock
Rais Donald Trump wa Marekani amemtaja muuaji wa watu 59 huku 527 wakijeruhiwa mjini Las Vegas kuwa mgonjwa aliye na akili punguani.
Akizungumza katika ikulu ya Whitehouse , amesema kuwa ataziangazia upya sheria za umiliki wa bunduki katika siku za usoni lakini hakuelezea zaidi.
Maafisa wa polisi wanajaribu kubaini kwa nini Stephen Paddock mwenye umri wa miaka 64 aliwafyatulia risasi watu waliokuwa katika tamasha akiwa katika ghorofa ya 32 karibu na hoteli ya Mandalay Bay.
Polisi walipata bunduki 23 katika chumba chake pamoja na vilipuzi.
Kufikia sasa hakuna sababu mwafaka iliotolewa na wachunguzi hawajapata ishara zozote za shambulio hilo kuhusishwa na ugaidi wa kimataifa.
Baadhi ya wachunguzi wamesema kuwa Paddock alikuwa na historia ya matatizo ya kiakili, lakini hilo halijathibitishwa.
Paddock hajakuwa na rekodi yoyote ya uhalifu na hakuwa akijulikana na maafisa wa polisi.
Mshukiwa wa mauaji ya las Vegas Stephen PaddockHaki miliki ya pichaFAMILIA YA PADDOCK
Image captionMshukiwa wa mauaji ya las Vegas Stephen Paddock
Akizungumza na wanahabari wakati alipokuwa akijiandaa kupanda ndege ya rais, bwana Trump alisema kuwa Paddock ni mgonjwa wa kiakili .
''Ana matatizo chungu nzima, na tunamchunguza kwa kina'' .
Alipoulizwa, bwana Trump alikataa kuliita shambulio hilo ugaidi wa nchini.
Kuhusu swala la udhibiti wa bunduki, rais alisema: Tutakuwa tukizungumzia kuhusu sheria za bunduki siku sijazo.
Rais Trump ambaye mipango yake kuhusu udhibiti wa bunduki umebadilika katika miaka ya hivi karibuni hakutoa maelezo zaidi.

No comments: