Tabia Mbaya Za Fedha Zinazowaacha Wengi Kwenye Umaskini



Idadi kubwa ya watu linapokuja suala la pesa, wapo makini sana na tabia kama kupanga mipango mizuri, kutumia pesa kwa busara na hata ikiwezekana kubana matumizi ili kuhakikisha usalama wa pesa unakuwepo.
Lakini, hata hivyo pamoja na wengi kijitahidi kufanya hivyo, bado zipo tabia ambazo watu wanazo zinawaacha au zinasababisha wengi kuendelea kubaki kwenye umaskini ingawa ukiangalia pia watu hao wana uwezo wa kupata pesa kila wakati.
Kwa hiyo hapa unaona tatizo la watu wengi sio kupata pesa, kama ni pesa kweli wanazipata, ila shida inakuja kwa kukumbatia tabia hizo ambazo zinawarudisha nyuma sana na matokeo yake kuwaacha katika dimbwi la umaskini.
Leo hapa katika makala haya, tunakuletea tabia mbaya ambazo kwa mtu yeyote akiwa nazo ni lazima mtu huyo ataendelea kubaki kwenye umaskini. Hakuna ujanja katika hili, kama una tabia hizi, nimesema utaendelea kubaki kuwa maskini.
1. Kushindwa kuweka kumbukumbu ya matumizi yako.
Haijalishi unakipato kikubwa au una kipato kidogo, kuandika matumizi yako ni jambo la lazima ili uweze kufanikiwa. Kitendo cha kuwa na kumbukumbu na matumizi yako si suala la kumwachia Bill Gates peke yake hata wewe linakuhusu.
Huhitaji kutumia pesa zako tu hovyo kwa sababu eti unazo, unachotakiwa kujua ni wapi kila pesa yako inakwenda. Zoezi hili litakusadia sana kuwa makini na pesa zako na kukuokolea pesa nyingi ambazo zingepotea bila sababu.
Hili jambo liko wazi, hutaki kuweka kumbukumbu zako vizuri, utake usitake huwezi kutoka kwenye umaskini hata ufanyeje. Kama unabisha wafatilie watu wenye pesa nyingi sana, utaona hili wanalifanya sana maishani mwao.
2. Mhemko wa matumizi.
Tunaposema mhemko wa matumizi ni kufanya matumizi ya pesa kwa kutawaliwa na hisia zako. Hapa unakuwa unafanya matumizi kwa kuongozwa sana na hisia na unakuja kushituka kile kipindi ambacho pesa zako zimekwisha.
Kwa mfano, kwa sababu una pesa kila kitu kinachopita machoni mwako unataka unanunue, zizikipita nguo unataka kununua, kikipita kitu hiki au kile unataka kununua pia, huu ndio mhemko wa matumizi tunaouzungumzia hapa na ni tabia mbaya ya kipesa..

No comments: