Shamsa Ford afunguka baada ya mume wake kuchepuka


Muigizaji wa filamu bongo Shamsa Ford ambaye ni mke wa mfanyabiashara wa mavazi Rashid maarufu kwa jina la Chid Mapenzi, amewajia juu wanaoingilia kati ndoa yake baada ya tetesi za mume wake kuchepuka, wakimtaka kuchukua hatua kwa haraka na kumuacha.
Kwenye ukurasa wake wa instagram, Shamsa ameandika ujumbe akieleza ni kiasi gani anampenda mume wake huyo na kumfurahia pale anapoomba msamaha akikosea, huku akisema hatokuja kumuacha mume wake hata kama amemsaliti.
"Mume wangu nikikuelewa mimi inatosha wengine wakipiga kelele tuchukulie kama burudani tu, jamani sitokuja kumuacha mume wangu kwa ajili ya mwanamke hata siku moja labda afanye makubwa yasiyoeleweka kwenye jamiii. Amecheat Bili Clinton sembuse Rashid wangu", ameandika Shamsa.
Hivi karibuni shamsa aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram, akisema kwamba anaona kuna 'jini mkata kamba' anainyemelea ndoa yake, na ndipo zilipofuatia taarifa za mume wake kusaliti ndoa na kuwa na mchepuko.

No comments: