Mbunge mmoja kutoka Uingereza Sir Nicholas Soames amelazimika kujitetea baada ya taarifa kuibuka kuhusu mkutano wake binafsi na Rais Robert Mugabe akiwa ziarani Zimbabwe.
Mbunge huyo mkongwe wa chama cha Conservative alikutana na Bw Mugabe wiki iliyopita.
Amesema alikutana na kiongozi huyo kukumbuka mchango wa babake ambaye alikuwa gavana wa mwisho wa taifa hilo lilipokuwa linafahamika kama Rhodesia Kusini.
Sir Nicholas amesema walikutana kujikumbusha mambo ya zamani na kuongheza kwamba: "Ilikuwa zaidi kwa sababu ya kukumbuka mambo ya zamani na ninafurahia hilo."
Lakini mbunge wa Labour Kate Hoey amesema ziara hiyo ni pigo kubwa kwa watu ambao wameteseka chini ya utawala wa Mugabe.
Kiongozi huyo wa miaka 93 amenukuliwa katika magazeti Zimbabwe akisema kwamba ziara hiyo ya Sir Nicholas ni ishara kwamba Waingereza wanataka mazungumzo na taifa lake.
No comments: