Kocha Salum Mayanga aomba msamaha kwa Watanzania


Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Mayanga amewaomba radhi mashabiki wa soka nchini kwa matokeo yasiyo mazuri kwenye mechi dhidi ya Malawi iliyopigwa Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam.
Mayanga amesema anayafanyia kazi mapungufu na kuahidi kuwa timu itafanya vizuri katika michezo inayokuja. “Naomba mashabiki watusamehe kwa matokeo ya mchezo uliopita, nimeyaona mapungufu ya timu na nitayafanyia kazi ili tuweze kushinda kwenye mechi zijazo”.
Aidha Mayanga ameeleza nia yake ya kupata michezo miwili ya kirafiki ili kujiweka vyema na mchezo wake wa kuwania kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Uganda Machi 2018.
Taifa Stars imekuwa haina mwendelezo wa matokeo mazuri ambapo ikumbukwe kuwa iliifunga Malawi kwenye michuano ya COSAFA lakini imeshindwa kufanya hivyo kwenye uwanja wa nyumbani.
Tanzania ipo Kundi L na timu za Uganda, Cape Verde na Lesotho kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019 nchini Cameroon.

No comments: