Neymar, Dybala na Kante watajwa kuwania Ballon d’Or 2017


Wachezaji watano wa kwanza watajwa kati ya wachezaji 30 watakao wania tuzo ya (Ballon d’Or 2017).
Majina ya wachezaji hao watano wa kwanza ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazili na klabu ya Paris Saint-Germain, Neymar, Paulo Dybala na N’Golo Kante wametangazwa mapema hii leo kuwania tuzo hiyo ya Ballon d’Or 2017.
Beki wa Real Madrid, Marcelo na mchezaji mwenzake Luka Modric pia ni miongoni mwa waliyotajwa.
Neymar amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya taifa ya Brazili na klabu ya Barcelona kabla ya kuuzwa katika kipindi cha majira ya joto na kuhamia PSG kwa dau lililoweka rekodi ya dunia ya paundi milioni 222.
Nisawa na Dybala ambae amekuwa msaada mkubwa ndani ya timu ya Juventus mwaka huu wa 2017.
Wakati Kante akifanikiwa kuisaidia klabu ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza kufanya vizuri.
Marcelo ametoa pasi tisa zilizochangia magoli ‘assists’ mwaka 2017 na Modric, wakiwa wameisadia Madrid kushinda kombe la Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ huku wakiiwezesha timu hiyo kutwaa kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Bado majina yataendelea kutajwa huku Cristiano Ronaldo ambaye anashikilia taji hilo akisubiriwa kwa hamu na Lionel Messi akiwa ni miongoni mwa wanao subiriwa lakini pia wapo wachezaji kama Antoine Griezmann na Gianluigi Buffon ambao nao bado na wanatarajiwa kuleta upinzani mkubwa katika tuzo hiyo.
Tutaendelea kukujuza kadri idadi ya wachezaji watakavyoweza kutajwa.
Majina matano mengine wanao wania tuzo ya Ballon d’Or 2017 ni wachezaji Suarez, Ramos, Oblak, Coutinho, Mertens
Tutaendelea kukujuza kadri idadi ya wachezaji watakavyoweza kutajwa.

No comments: