Msanii wa Bongo Flava, Aslay amesema moja ya ndoto zake ni kupeleka muziki wake kimataifa.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Natamba’ ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa anaona muziki wake kwa upande wa nyumbani umeshakubalika hivyo mipango yake siku za mbeleni kufanya hivyo.
“Nataka nivuke kimataifa, unajua siwezi kufanya muziki tu nipo nyumbani, kwanza naogopa kuzoeleka na watu nataka nivuke kimataifa baadae niwe na maisha yangu ambayo naweza kusema namsaidia mtu akatoboa sehemu fulani,” amesema Aslay.
Ameongeza kuwa anaamini kutoboa kimataifa kutamuimarisha kisanii na kiuchumi hivyo ataweza kuwasaidia vijana wengine wenye viapaji kupitia label yake ambayo ipo tayari kwa sasa.
No comments: