Akizungumza mara baada ya kuapishwa kwa Mawaziri wapya walioteuliwa na Rais Magufuli, Job Ndugai amesema hatomsahau katibu huyo, huku akimkaribisha Katibu mpya aliyeteuliwa.
“Namkaribisha sana Katibu wa Bunge mpya bwana Kigaigai, karibu sana Dodoma, na kwa fursa hii niliyopata nimshukuru sana Katibu wa Bunge anayemaliza muda wake, Dkt. Thomas Kashilila ahsante sana kwa utumishi uliotukuka, tunakushukuru sana hatutokusahau”, amesema Spika Ndugai.
Uteuzi wa Katibu mpya wa Bunge umefanyika Oktoba 7, 2017, ambapo Rais Magufuli amemteua Steven Kigaigai kuwa Katibu wa Bunge, na aliyekuwa akishika wadhifa huo Dkt. Thomas Kashilila, kutarajia kupangiwa kazi nyingine ya kufanya.
No comments: