Habari nzuri kwa mashabiki wa simba


Kamati maalumu ya kusimamia mchakato wa zabuni ya kumpata muwekezaji kwenyemuundo mpya wa klabu ya Simba imeelezea maendeleo yake tangu kuanzishwa kwake baada ya Mkutano Mkuu uliyofanyika Agosti 20 mwaka huu.
Mwenyekiti wa kamati ya zabuni Jaji Thomas Mihayo akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Bw. Abdul-Razaq Badru wakati kamati hiyo ilipokuwa ikiwasilisha taarifa ya kuanza rasmi kwa mchakato wa uwekezaji katika klabu ya Simba kwa waandishi wa habari.
Kamati ya Zabuni imekutana na kupitia nyaraka mahususi kwa ajili ya kupata ufahamu na kukusanya taarifa na takwimu muhimu huku ikikutana na kushauriana na kamatia ya utendaji pamoja na wadau na wataalam kadhaa na kuandaa mwaliko wa awali kwa ajili ya wanachama na taasisi zenye nia na sifa za kushiriki katika mchakato wa Zabuni.


Kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa tarehe 20/08/2017 azimio la kuanzisha na kutekeleza mchakato wa uwekezaji ilipitishwa.
Baada ya azimio hilo hatua kadhaa zimeazimishwa, moja wapo ni uteuzi wa kamati ya Zabuni ambayo inawajibika kusimamia mchakato wa kizabuni kwaajili ya kupata mwekezaji mwenye sifa kama zilivyoanishwa.
Tangu kuteuliwa kwake, kamati ya Zabuni imekutana na kupitia nyaraka mahususi kwa ajili ya kupata ufahamu na kukusanya taarifa na takwimu muhimu.
Aidha kamati imekutana na kushauriana na kamatia ya utendaji pamoja na wadau na wataalam kadhaa na kuandaa mwaliko wa awali kwa ajili ya wanachama na taasisi zenye nia na sifa za kushiriki katika mchakato wa Zabuni.
Kupitia taarifa hii, kamati ya Zabuni inatamka kwamba nyaraka za mwaliko wa awali (Expression of Interest) ziko tayari. Wawekezaji wenye sifa na vigezo wanaweza kuzipata. Mwaliko wa kuchukua nyaraka hizi(Eol) utatangazwa katika vyombo vya habari kwa muda wa siku 10 ilikuwapatia fursa ya kutosha wazabuni watarajiwa kujiandaa. Kukamilisha nyaraka muhimu na kufanya mashauriano kabla ya kuwasilisha.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha nia ya kushiriki katika mchakato wa kiuwekezaji itakuwa Octoba 18,2017 saa 8 alasiri.




No comments: