Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), Bw. Ahmad Ahmad leo Oktoba 9, 2017 amepokea ugeni kutoka Tanzania, Rais wa TFF Bw. Wallace Karia na Kaimu Katibu Mķuu, Bw. Kidao Wilfred waliotembea Makao Makuu ya CAF yaliyoko Cairo, Misri.
Rais wa Heshima wa TFF ambaye ni Mjumbe Kamati ya Utendaji ya CAF, Bw. Leodegar Tenga pia alishiriki katika mkutano huo ambao Rais wa CAF alithibitisha msaada TFF katika mipango ya maendeleo ya Tanzania kwa kuwa soka siku zote hujenga umoja.
Pata habari za Michezo kiganjani mwako kwa kudownload hapa. USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA,BOFYA KITUFE KILICHOANDIKWA LIKE
No comments: