Hali ya Mlinda mlango wa klabu ya Simba Said Mohamed "Nduda" ambae kwa sasa yupo nchini India ambako alikwenda kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa goti imeripotiwa kuimalika baada ya upasuaji kumalizika salama.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia ni kua mlinda mlango huyo tayari ameanza mazoezi mepesi ya viungo huku taarifa hizo zikiarifu kuwa mlinda mlango huyo ameupongeza uongozi wa klabu ya Simba na kutaka uongozi pamoja na wana chama kumuombea ili apone na arejee dimbani mapema.
Nduda aliumia mazoezini wakati klabu hiyo ilipokua ikijiandaa kuwavaa mahasimu wao, klabu ya Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

No comments: