Ikiwa leo ni Birthday ya Zari The Boss Lady, Diamond amechukua muda wake na kuandika ujumbe kwa Baby Mama huyo ikiwa ni sehemu ya pongezi zake kwake.
Ujumbe huo ambao ameundika katika mtandao wa Instagram amemtaja Zari kama mwanamke ambaye amekuwa naye bega kwa bega katika mafanikio yake.
Uzuri na Urembo pengine ningetembea nikakuta baadhi wanao pia… Lakini Akili, Hekma, pamoja na Roho yako ya kwenye Shida na Raha kwangu ndio kitu pekee kinachonifanya nikupende na kukuthamini zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda…… wanaposema kwenye kila Mafanikio ya Mwanaume kuna Mwanamke imara nyuma, hawamaanishi eti anaepika na kuosha vyombo sana ama kufua nguo kila siku… Hapana! ni mwanamke Mwenyekuwa bega kwa bega na Mpenzie kwenye Shida na Raha… Happy birthday General
Wiki hii wawili hao wamekuwa wakiripotiwa kutoelewana baada ya Diamond kuweka bayana kuwa alizaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto wakati bado yupo katika mahusiano na Zari.
No comments: