Kipindi cha ujauzito kwa mama ni kipindi muhimu sana ambacho kwa wakati huu mama hatakiwi atumie kitu chochote cha kujitibu bila ushauri wa daktari kwani kinaweza kudhuru mtoto lakini pia kipindi cha ujauzito ni kipindi ambacho mama hatakiwi kunywa kileo chochote kile unachokifahamu.
Sio bia, sio spirit, wala mvinyo au wine. wanawake wengi wa siku hizi hubeba mimba bila kufahamu kwamba wana mimba na huja kugundua baada ya mwezi mmoja au miwili baada ya kumshindilia mtoto pombe za kutosha.tabia hii ina madhara makubwa sana kwa mama na mtoto kama ifuatavyo...
1. Mtoto kua na umbo la ajabu; mtoto huweza kuzaliwa na kichwa kidogo, uso kama bapa na macho madogo sana. dalili hizi huweza kuanza kuonekana katika umri wa miaka 2 na mara nyingi mtoto hua tofauti na wenzake.
2. Kuchelewa kukua; pombe huingilia mfumo wa ukuaji na kumchelewesha mtoto kufanya baadhi ya mambo kama kutambaa, kutembea, kuongea na kadhalika. ukimuangalia mtoto mwenye umri kama huo huo ataonekana mkubwa kuliko huyu anayetumia pombe.
3. Kushindwa kujifunza; mara nyingi watoto hawa hua wabovu sana darasani na kushindwa kuelewa vitu kama watoto wengine..mata nyingi mzazi huishia kulalamika na kumshangaa mtoto na kumuona mzembe bila kujua chanzo ni yeye...
4. Kuchelewa kula kwa mtoto; kawaida mtoto anatakiwa anywe maziwa tu kwa muda wa miezi sita, tena maziwa ya mama baada ya hapo aanze kula chakula. mtoto aliyepata madhara ya pombe hushindwa kunyonya na kuchukua muda mrefu sana kuanza kula.
5. Matatizo ya viungo; siku hizi kuna picha zinatumwa sana mitandaoni zikionyesha mtoto kazaliwa bila mikono, miguu au kaunganikana kichwa na pacha mwenzake. hizo sio bahati mbaya kama watu wanavyodhani ila hayo ni madhara ya vitu ikiwemo pombe.
6. Kuharibika kwa ujauzito; pombe inaweza kuingilia mfumo wa homoni za mwanamke au kufungua mlango wa uzazi na kusababisha kuharibika kwa mimba, mimba huweza kuharibika ghafla au taratibu kulingana na aina ya pombe.
7. Kuzaa kabla ya muda; kwenye mimba kubwa pombe inaweza kusababisha kuanza kwa uchungu kabla ya muda na kumzaa mtoto ambaye hajakomaa maarufu kama kabichi.
Mwisho; hakuna kipindi ambacho ni salama kunywa pombe kipindi cha ujauzito, kama hauhitaji mtoto kwa sasa tumia vizuizi vya mimba lakini kama unakunywa pombe na kufanya ngono bila kinga utajikuta una mimba ambayo imeshaathirika na pombe tayari na ukipata mimba acha pombe kabisa.
No comments: