KWA NINI COCA COLA SI NZURI KWA MATUMIZI YA BINADAM....Soma hapa

Image result for COCA COLA IMAGE
Coca-Cola ni kinywaji maarufu na kinajulikana sehemu nyingi sana duniani.

Kuna maswali mengi ya kujiuliza juu ya unywaji wa kinywaji hiki kwa binadamu,kama ni sahihi kwa matumizi ya binadamu au la,au unywaji wa kinywaji hiki una madhara kwa baadae au la, nauliza hivi kwa sababu pH yake ipo juu kuliko hata ya asidi ya kwenye betri.

Taasisi ya moyo,mapafu na damu walidhamini utafiti ufanywe kwa mtu mmoja mmoja ambae anatumia japo soda moja kwa siku.

Walikutwa na uwezekano wa asilimia 44 ya kupata magonjwa yanayohusiana na mishipa ya moyo na aina ya pili ya kisukari kwa mda wa miaka minne

Utafiti ulifanywa kwa watu zaidi ya 2400 ya vijana,ambapo watu 1600 walikuwa hawana dalili zozote za metabolic syndrome ,na baada ya miaka minne nao wakawa na uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na kisukari.

Watu wanaopendelea kutumia soda kila siku wanaweza kupata matatizo ya;

1.uwezekano wa kupata shinikizo la damu

2.asilimia 25 walikuwa na uwezekano wa kupata kisukari

3.asilimia 30 walikuwa na uwezekano wa kuongezeka uzito

4.asilimia 31 walikuwa na uwezo wa kupata obesity

Utafiti mwingine unaonyesha asilimia 48 wanaotumia kinywaji hiki iwe mara kwa mara au mara chache wana uwezekano mkubwa wa kupata shambulio la moyo au stroke.

Pia utumiaji wa vinywaji baridi umethibitika kuongeza hatari ya matatizo ya kupumua kama asthma na COPD

Matumizi 5 ya Coca-cola

Tambua kuwa unywaji wa Coca-Cola utakuletea madhara katika afya yako,basi ni nzuri zaidi kwenye matumizi ya kusafishia
Coca-cola unaweza kuitumia kwa matumizi ya nyumbani kama;
  1. 1.kusafisha choo
  2. 2.kusafishia injini
  3. 3.Kuondoa kutu
  4. 4.Kuondoa oil iliyomwagika sakafuni
  5. 5.Kuondoa madoa ya damu kwenye nguo au kitambaa

No comments: