Wazee Lindi wapata vitisho juu ya tofauti za itikadi za kisiasa
ASIYE SIKIA la mkuu huvunjika guu. Ndivyo tunavyoweza kuchukua na kuitafsiri tahadhari iliyotolewa na wazee wa mkoa wa Lindi kwa wanachi nchini.Waliyotoa wakati wa mkutano wa baraza la wazee la mkoa wa Lindi,uliofanyika leo kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa iliyopo katika manispaa ya Lindi.
Wakizungumza kwenye mkutano huo,wazee hao waliotoka katika wilaya za mkoa huu walisema tofauti za itikadi za kisiasa zinazojitokeza nchini hazina mwelekeo wa kuwaunganisha wananchi.Badala yake zimeanza kuleta mpasuko hata kwa wazee.Ambao kimsingi wanatakiwa kuwa waonyaji,washauri na wakemeaji wa matendo yanayoweza kuharibu umoja na mshikamano uliodumu miaka mingi.
Mzee Yusufu Kisamile kutoka wilaya ya Kilwa,alisema tofauti za itikadi za kisiasa katika wilaya hiyo zimeanza kuharibu mshikamano na upendo uliodumu miaka nenda,miaka rudi.Huku hali ya mgawanyiko ikiongezeka siku hadi siku.
Mzee Kisamile alisema hali hiyo imesababisha hata wazee kuanza kuhitilafiana na kushindwa kutimiza wajibu wao wa msingi katika jamii wakushauri,kuonya na kukemea mambo yanayoweza kuvuruga umoja.
"Tangu kuingia mfumo wa vyama vingi hali ilianza kubadilika,wazee hatuaminiani na hatushauri wala kuonya.Sababu tumesimama katika itikadi za siasa kuliko nafasi yetu katika jamii,hata mabaraza yanaonekana ya vyama vya siasa wakati hakuna ukweli wowote. Sifa ya mabaraza aya ni uzee,nilazima tubadilike tuungane tuweke siasa pembeni,Kilwa tumekwama sana,"alisema mzee Kisamile.
Mzee Abdallah Majumba aliyetoka katika wilaya ya Lindi,ambae pia ni mwenyekiti wa mkoa wa baraza hilo,alisema wanasiasa nichanzo cha mgawanyiko ulioanza kujitokeza nchini.Kwamadai kuwa baadhi yao wanawatumia wanajamii ikiwamo wazee kama madaraja ya kuvukia ili kufikia masilahi yao ya kisiasa.
Mzee Majumba alitoa wito kwa wazee wote nchini kutoyumbishwa na wanasiasa.Badala yake waoneshe mshikamano nakukemea bila woga mambo yanayoweza kuvuruga amani ya nchi bila kujali wanaofanya hivyo wanatoka katika vyama gani cha siasa.Huku akitahadharisha kuwa wasipofanya hivyo watakuwa wamejiondolea thamani ya uzee wao.
"Leo tunashuhudia jaziba na mihemko kutoka kwa wanasiasa, mtu anashabikia hata mambo yanayochochea vurugu kwasababu anaefanya hayo ni kiongozi au mwanachama wa chama anachokipenda.Bila kujali madhara ya kauli na vitendo vya mtu huyo lakini tupo kimya,"alishanga Majumba.
Kauli za wazee hao wawili ziliungwa mkono na mzee mwingine, Nicodemus Sanga,aliyesema kunahaja ya kuimarisha mabaraza nakuyatambua kuwa nisehemu muhimu ya kujenga maadili mema kwa jamii.Lakini pia yasihusishwe na itikadi za siasa,dini na ukabila.
Nae ofisa wa maendeleo ya jamii wa mkoa wa Lindi,Anna Maro alisema upo uwezekano mkubwa wa kupungua migogoro katika jamii iwapo wazee watatimiza wajibu wao wa kushauri na kukemea mambo yasiyofaa kutendwa kwa ajili ya mshikamano,utulivu na amani.11:Alisema kitendo cha wazee kuanza kujitenga nakuacha wajibu huo kwa viongozi wa dini na serikali kinapunguza nguvu za pamoja za kujenga maadili mema kwa jamii.
Kwa upande wake,ofisa utumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi,Neema Konzo,ambae katika mkutano huo alimwakilisha katibu tawala wa mkoa wa Lindi, alisema serikali inatatambua thamani na umuhimu wa wazee katika ujenzi wa uchumi,maendeleo ya nchi na maadili mema.Akibainisha kwamba kwakuzingatia ukweli huo imekuwa bega kwa bega nao.
" Kuthibitisha hilo kwavitendo,katibu tawala wa mkoa huu amewapa chumba kimoja katika jengo hili mtumie kwa kazi za ofisi,"Konzo alisema na kuibua shangwe ukumbini humo.13:Wajumbe wa mkutano huo walimchagua Mzee Abdallah Majumba kuendelea na wadhifa wake wa uenyekiti wa mkoa.Ambapo aliyechaguliwa kwa nafasi ya ukatibu ni Denis Mahundu.
No comments: