Manji anatumia vidonge 30 kwa siku – Daktari Magereza

Hukumu ya kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji itasomwa October 6 mwaka huu baada ya mahakama ya Kisutu kupitia Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha kufunga kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi
Image result for picha za manji
Waliotoa utetezi wao leo ni pamoja na sekretari wa Manji, Maria Rugarabamu , daktari Mkuu wa Zahanati ya Gereza la Keko, Inspector Eliud Mwakawanga, pamoja na Daktari Bingwa wa Afya ya akili na dawa za kulevya, Francis Benedict kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke ambapo kila mmoja aliieleza mahakama kile anachokijua kuhusu tuhuma za mfanyabiashara huyo kutumia dawa za kulevya.
Mahakama ilipokea risiti za dawa ambazo alikuwa anaandikiwa Yusuf Manji na ofisi ya Mganga Mkuu wa Zahanati Magereza ya Keko, Inspector Eliud Mwakawanga kama vielelezo kwa upande wa utetezi.
Mganga huyo amesema Manji alikuwa anatumia vidonge 30 kila siku ili kuimarisha afya yake.
Alisema kuna wakati ambao Manji alikuwa anaamka akiwa kama amechanyikiwa lakini akimpatia dawa anarudi katika hali yake ya kawaida.
Kwa upande wa shahidi wa tatu ambaye ni Daktari Bingwa wa Afya ya Akili na Dawa za Kulevya kutoka hospitali ya Rufaa ya Temeke, alisema kuna baadhi ya madawa ya hospitali akitumia mgonjwa mkojo wake ukipimwa utakutwa na chembe chembe za Morphiem ambazo pia hupatikana katika mkojo ya watu wanaotumia dawa za kulevya.
Naye shahidi wa kwanza siku ya leo Maria Rugarabamu ambaye ni sekretari wa mfanyabiashara huyo, aliithibitisha mahakama kupokea barua ya uthibitisho kutoka kwa daktari wa Manji kutoka Marekani ambaye alikuwa akimwandikia dawa Manji ambazo ndani yake zinadaiwa kuwa na cheche za Morphiem

No comments: