Wanandoa wakiri kuua watu 30


Wanandoa waliokamatwa kwenye mji ulio kusini magharibi mwa Urusi wa Krasnodar, wamekiri kuwaua hadi watu 30.

Dmitry Baksheev, 35, na mke wake Natalia, walimatwa baada ya mwili uliokuwa umekatwa katwa ulipatikana kwenye kambi ya jeshi ambapo wawili walikuwa wanaishi.

Polisi walithibitisha kuwa bidhaa kadhaa za chakula na nyama vilivyopatiakan nyumbani kwao vinachunguzwa ikiwa vina DNA ya binadamu.


Simu ya mkononi ilipatwa na wajenzi wa barabara mapema mwezi huu ikiwa na picha za miili iliyokuwa imekatwa katwa.

Picha moja iilyochapishwa na vyombo vya habari nchini Urusi ilmuonyesha Bw Baksheev akiwa sehemu ya mwili wa binadamu kwenye mdomo wake.

Mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 35 kisha uliripotiwa kupatikana katika chuo cha kijeshi ambapo wawili hao wanaishi.

Mwili huo ulikuwa umekatwakatwa na mkoba ulio na bidhaa za muathiriwa nao ulipatikana.

Wizara ya mambo ya ndani nchini Urusi ilithibitisha kuwa mwanamume aliye kwenye picha hizo ametambuliwa na kukamatwa.

Picha zimetolewa kwa vyombo vya habari nchini Urusi zinazoripotiwa kuonyesha polisi wakisaka nyumba ya wawili hao.

Vipande kadha vua miili ya binadamua vilionyeshwa kwenye picha vingine vikiwa ndani ya ndoo.

Vyombo vya habari vinasema kuwa picha zilizopatikana zimechapishwa kwenye ukuta na kwenye simu zilionyesha kuwa mauaji hayo huenda yalianza karibu miongo miwili iliyopita.

Picha moja ni ya tarehe 28 Disemba mwaka 1999 na inaonyesha kichwa cha binadamu kikiwa kwenye sahani pamoja na tunda.

No comments: