MKUU wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ametoa onyo kali huku akiawaagiza wanajeshi kuacha kujihusisha na matumizi mabaya mitandao ya kijamii kwani kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za jeshi.
Jenerali Mabeyo amesema hayo leo Jumamosi katika hafla ya kutunuku nishani ya Luteni Usu kwa maofisa 422 wa jeshi iliyofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Amesema jukumu la wanajeshi ni ulinzi wa Taifa hivyo kujiingiza katika mambo yasiyofaa ni ukiukwaji wa taratibu za jeshi hilo.
Mabeyo amewataka wanajeshi kuepuka kuliingiza jeshi kwenye siasa na badala yake wanatakiwa kuwa na uzalendo kwa Taifa lao.
“Niwasihi msimame kwenye kiapo mlichoapa leo. Wapo baadhi ya askari husahau kwa haraka na kukiuka kiapo, msifike huko. Matamshi uliyoyatoa leo yanaelekeza wajibu wako, utii, kuilinda katiba, kumtii Rais na kumtumikia.” alisema Mabeyo.
No comments: