Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo vya Ritcher limesikika nchini Korea Kaskazini.
Tetemeko hilo lilitokea kilomita 50 kutoka kituo cha majaribio ya makombora ya kinyuklia .
Mitetemeko mengine ya ardhi imetokea wakati wa majaribio ya makombora.
Wataalam wa mitetemeko nchini China wamesema kuwa wanatuhumu ulikuwa mlipuko.
Lakini Korea Kusini inasema kuwa huenda ni tetemeko la kawaida ambalo halikusababishwa na jaribio la kombora la kinyuklia.
Korea Kaskazini ilifanya majaribio makubwa ya kombora lake la kinyuklia mnamo Septemba 3 ambalo limeshutumiwa pakubwa katika mkutano wa umoja wa mataifa.
Kiwango cha tetemeko la siku ya Jumamosi ni kidogo ikilinganishwa na wakati taifa la Korea Kaskazini linapofanyia majaribio makombora yake.
No comments: