Utafiti: Idadi ya watu wazima waathirika wa virusi vya HIV yaongezeka Ulaya
Idadi ya watu wazima ambao wanagunduliwa kuwa na virusi vya HIV kote barani Ulaya inazidi kuongezeka, kwa mujibu wa utafiti.
Watafiti kutoka kituo cha kukabiliana na magonjwa cha Ulaya waliangalia matokeo ya vipimo kutoka nchi 31 kati ya mwaka 2004 na 2015.
Waligundua kuwa mwaka 2015, karibu kisa kimoja kati ya visa vipya sita vilikuwa miongoni mwa watu walio na zaidi ya maika 50, ikilinganishwa na kisa kimoja kati ya visa 10 miaka kumi iliyopita.
Uchunguzi huo unazitaja nchi 16 zikiwemo Uingereza na Ujerumani kuwa zile zinazoshuhudia kuongezeka kwa visa vya watu walio na zaidi ya 50 wanaoambukizwa ugonjwa wa HIV.
Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la Lancet pia uligundua kuwa watu wazima, wana uwezekano wa kupatikana na ugonjwa wa HIV, ambao umefika viwango vya juu ulio vigumu kutibu.
Hata hivyo uchunguzi huo hakuangalia kuhusu ni kwa nini watu wazima wanambukizwa sana na ugonjwa huo. Lakini uligundua kuwa maambukizi ni kupitia mapenzi ya watu wa jinsia moja na kuwa wanaume zaidi wanaambukizwa ugonjwa huo kuliko wanawake.
Uchunguzi huo ulitaka kuwepo hamazisho zaidi na watu kupimwa hasa wale walio na zaidi ya miaka 50.
Vijana bado ndio wengi wanaopata maambukizi mapya ya ugonjwa wa HIV huku zaidi ya watu 300,000 walio kati ya miaka 15 na 49 wakipatikana na ugonjuwa wa hiu kote ulaya katika kipindi cha miaka 12 ya utafiti huo ikilinganishwa watu 54,000 wazee.
No comments: