MEYA wa Manspaa ya Ubungo, Bonface Jacob amesema anakabiliwa vitisho na vishawishi mbalimbali ili kuhakikisha anafuta kesi aliyoifungua dhidi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ya kughushi vyeti,Hata hivyo, hakuweka bayana anapokea vitisho kutoka kwa nani pamoja.
RC Makonda anatuhumiwa kudanganya na kutumia vyeti ambavyo siyo vya kwake, na kwamba yeye jina lake alilopewa na wazazi wake ni ‘Daudi Albert Bashite’
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kutoka kwenye ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma amesema kuwa Mkuu wa Mkoa huyo amekiuka sheria za utumishi wa umma.
Amesema kuwa tayari kuna viashiria vya ushawishi kutoka kwa watu wa Makonda wanaotaka akubali kuondoa shauri hilo.
Ametaja vitisho anavyokabiliana navyo ni pamoja na kusingiziwa kwamba anatumia ofisi kufanya mikutano ya kisiasa.
TAZAMA HAPA
No comments: