Upelelezi kesi ya Aveva, Kaburu umekamilika, kilichoamualiwa?

 Image result for aveva wa simba

Upelelezi wa awali katika kesi ya utakatishaji fesha inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa leo September 18, 2017 kuwa, upelelezi wa awali wa kesi hiyo umekamilika ambapo jalada la kesi limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili alisome na kueleza kama anaona umekamilika au la.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi September 27, 2017.

No comments: