Hii ndo list ya watu wanaosubiri kunyongwa tanazania


IDADI ya Watanzania wanaosubiri kunyongwa imezidi kuongezeka na kufikia 467 kutokana na hukumu ya kifo kutotekelezwa tangu mwaka 1994.

Ripoti iliyotolewa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika mafunzo kwa waandishi wa habari mjini Morogoro hivi karibuni, ilibainisha kuwa hakuna hukumu yoyote ya kifo iliyosainiwa na Rais ili kutekelezwa hadi Oktoba 2015.

Ripoti hiyo ya Mpango wa Kujitathmini Kuhusu Hali ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu (UPR), unaotekelezwa kwa mara ya pili nchini, ilionyesha kuwa kuna mahabusu 465 wanaosubiri adhabu ya kifo, kati yao wanaume ni 445 na wanawake ni 20.

Haya hivyo, idadi hiyo iliongezeka jana, baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa, kuwahukumu watu wawili wakazi wa Kijiji cha Kaengesa wilayani Sumbawanga kunyongwa hadi kufa, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanamke na kumsababishia kifo.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Dk. Adamu Mambi, baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi wanne.

Kutokana na hukumu hiyo sasa Watanzania wanaosubiri magerezani kunyongwa imeongezeka kadi watu 467 huku wanaume wakiongezeka kutoka 445 na kufikia 447 na wanawake wakiendelea kubakia 20.

Waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa ni Maurus Semwanza na Edward Chikwema ambao walimbaka Magreth Lazaro kisha kumuingiza kitu chenye ncha kali katika sehemu za siri hadi utumbo kutoka nje.

Katika shauri hilo ambalo upande wa mashitaka waliongozwa na mawakili Njoloyota Mwashubila na Safi Kashindi, huku mshitakiwa akitetewa na Wakili Peter Kamyalile, Ilidaiwa washitakiwa walitenda kosa hilo Juni 10, mwaka 2012 katika Kijiji cha Kaengesa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.

Ilidaiwa siku ya tukio saa 4:00 usiku, mwanamke huyo akiwa katika moja na baa za pombe ya kienyeji, alitoka nje kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo ndipo washitakiwa hao walipomvamia na kumziba mdomoni na matambala kisha kumpeleka kichakani ambako walimbaka kisha kumuingiza kitu chenye ncha kali sehemu za siri na kumsababishia utumbo kutoka nje.

Ildaiwa baada ya kumfanyia ukatili huo walitokomea kusikojulikana, ndipo mwanamke huyo alipookolewa na wasamaria wema ambao walimpeleka katika Zahanati ya Kaengesa na baada katika Hospitali ya mkoa ambako alifariki dunia kutokana na kutokwa na damu nyingi.

Ilidaiwa na mawakili wa serikali kwamba mtuhumiwa kabla ya kufariki aliwatambua wabakaji hao kwa majina, hivyo polisi kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya dola.

Kabla kutolewa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Mwashubila aliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Akitoa hukumu Jaji Dk. Mambi alisema washtakiwa wamekutwa na hatia, hivyo kwa mujibu wa kifungu 196 sura 16 cha Sheria ya Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa marekebisho mwa 2002, washtakiwa wanahukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

No comments: