Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala amewasili wilayani Ngara na kuagiza kambi za wakimbizi za muda zifungwe kwa wanaotoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Amesema wageni watakaoingia wasiitwe wakimbizi bali watakuwa ni wahamiaji haramu.
Dk Makakala amesema leo Jumatano kuwa, Mkoa wa Kagera unapakana na Uganda, Rwanda na Burundi, hivyo wananchi wasioe raia wa kigeni kinyume cha utaratibu. Amesema ni lazima hati ya ukaazi ilipiwe
Kamishna Jenerali Makakala ameahidi kuongeza watumishi wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera.
Pia, ameiomba Serikali kutoa vifaa vya usafiri.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Michael Mntenjele alisema kuna watu 223 wanaoomba hifadhi kutoka Burundi na DRC ambao wanapokewa katika kambi ya Rumasi wilayani hapa.
Amesema changamoto iliyopo ni maeneo ya mipaka kuwa wazi na kutokuwepo askari wa kutosha kudhibiti raia wa kigeni ambao huingia kufanya kazi kwa Watanzania na baadhi hupata makazi na wengine kuolewa.
Pia, amesema vigingi vya mipaka vilivyowekwa tangu wakati wa ukoloni na vingine vya mwaka 2014 vinaingia kwenye mashamba ya wananchi.
Mkuu wa wilaya amesema walioolewa au kuoa wanakabiliwa na changamoto ya kukosa Dola 50 za Marekani za kulipia hati ya ufuasi.
No comments: