Seduce Me ya Alikiba yatua Marekani kwa Swizz Beatz

Muziki wa Bongo Flava kwa sasa umeanza kuchezwa takribani dunia nzima, hakuna ubishi kwenye hilo
Wiki hii umefanyika uzinduzi wa bidhaa za BallyXSwizz za mtayarishaji na msanii mkubwa wa Marekani Sizz Beatz, katika sherehe hiyo wimbo wa ‘Seduce Me’ wa Alikiba ulikuwa ni mipongoni mwa ngoma zilizochezwa na kufurahiwa zaidi.
Flaviana Matata alikuwa ni miongoni mwa mashabiki ambao wamehudhuria katika sherehe hiyo. Kupitia mtandao wa Twitter Matata ameweka kipande cha video hiyo na kuandika, “When you go to support a friend and his Dj plays Tz music @THEREALSWIZZZ thanks 4 supporting our artist @OfficialAliKiba #BallyXSwiss launch.”

No comments: