Manchester United itawakosa viungo wa kati Marouane Fellaini , Michael Carrick na Paul Pogba katika mechi ya Jumatano ya vilabu bingwa dhidi ya CSKA Moscow.
Fellaini ana jeraha la kifundo cha mguu baada ya Shane Long kumchezea visivyo katika mechi ya Jumamosi huko Southmpton.
Pogba hajacheza tangu mechi ya ushindi dhidi ya Fc Basel mnamo mwezi Septemba 12 kutokana na jeraha la mguu.
Carrick pia anauguza jeraha, huku beki Phil Jones akiweza kucheza baada ya kutumikia marufuku lakini hatoshiriki.
United ambayo haijafungwa katika mechi nane msimu huu na CSKA zote zilishinda mechi zao za ufunguzi katika kundi A.
Huku Manchester United ikiishinda Basel 3-0 katika uwanja wa Old Trafford ,klabu hiyo ya Urusi ilipata ushindi wa 2-1 ugenini Benfica nchini Ureno.
Mkufunzi wa United Jose Mourinho amesema kuwa kuwa jeraha la Fellaini lingekuwa baya zaidi, lakini anataraji kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji atarudi hivi karibuni.
''Fellaini alikuwa na bahati'', aliongezea.
''Sitokuwa na Fellaini, Sitokuwa na Pogba na pia hatutakuwa na Carrick, kwa hivyo viungo wakati wote watakosekana katika mechi hii'', alisema.
No comments: